Mfanyabiashara na mkandarasi kijana, Enock Zadock Koola, ashinda kwa kishindo kura za maoni Jimbo la Vunjo, kwa kupata kura 1999 Kati ya 4080.

Koola amewabwaga wenzie watano (5) wakiongozwa na mbunge anayemaliza muda wake Dk. Charles Kimei aliyepata kura 861 na kushika nafasi ya pili.
Hatimae sauti za wanavunjo zimesikika!Ushindi huu unaashiria mwanzo wa zama mpya za maendeleo kwa wana Vunjo. Hakika, historia imeandikwa kwa kishindo!
