Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeMichezoFadlu Davids aanika malengo mapya Raja Club Athletic

Fadlu Davids aanika malengo mapya Raja Club Athletic

Kocha Fadlu Davids ameanza rasmi maisha yake mapya ndani ya Raja Club Athletic ya Morocco na kuweka wazi matarajio yake makubwa—kubeba makombe, akianza na lile la Ligi Kuu ya nchi hiyo, maarufu kama Botola Pro League.

Katika mahojiano yaliyopakiwa kwenye ukurasa rasmi wa Raja, Fadlu amesema dhamira yake ni kuona klabu hiyo inapata mafanikio makubwa ndani na nje ya Morocco, akisisitiza kuwa hana sababu nyingine zaidi ya ushindi na heshima kwa mashabiki.

Mbali na kujiunga mwenyewe, Fadlu ameondoka na benchi lake lote la ufundi alilokuwa nalo akiwa Simba SC, ambao sasa wataanza naye ukurasa mpya Raja. Kikosi hicho cha benchi la ufundi kinaundwa na:

  1. Darian Wilken – Kocha Msaidizi
  2. Wayn Sandilands – Kocha wa Magolikipa
  3. Mueez Kajee – Video Analyst
  4. Durell Butler – Kocha wa Viungo

Mashabiki wa Raja sasa wanasubiri kuona namna kikosi hicho kipya cha ufundi kitakavyoweka chapa yake ndani ya Botola Pro League na mashindano mengine barani Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments