Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeMichezoFeisal Salum asaini kandarasi mpya Azam FC

Feisal Salum asaini kandarasi mpya Azam FC

Kiungo fundi Feisal Salum Abdallah ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Azam FC, hatua inayomfanya abaki Chamazi hadi mwaka 2027.

Feisal, ambaye ameendelea kuwa mhimili muhimu wa kikosi cha Azam katika misimu ya karibuni, amekuwa chachu kubwa ya mafanikio ya timu hiyo kutokana na uwezo wake wa kutuliza mchezo na kusambaza pasi za mwisho. Uongozi wa Azam umesisitiza kuwa nyota huyo ataendelea kuwa sehemu ya mikakati ya muda mrefu ya klabu hiyo katika kufukuzia mataji ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Kusaini kwa mkataba huo kunakuja wakati Azam FC ikiendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, huku ikijivunia wachezaji wake wenye uzoefu na chipukizi wanaoibuliwa kutoka akademi ya klabu hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments