Tuesday, March 31, 2026
spot_img
HomeMichezo‎FIFA yaja na mabadiliko mapya Kombe Dunia

‎FIFA yaja na mabadiliko mapya Kombe Dunia

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza mabadiliko matano mapya yatakayotumika katika Kombe la Dunia 2026, yakilenga kupunguza upotevu wa muda na kuongeza kasi ya mchezo.

‎Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, mchezaji anayefanyiwa mabadiliko atalazimika kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10. Endapo atachelewa, mchezaji anayetarajiwa kuingia atalazimika kusubiri kwa dakika moja kabla ya kuruhusiwa kuingia uwanjani.

‎Aidha, mipira ya kurusha pembeni pamoja na golikiki italazimika kuanzishwa ndani ya sekunde tano. Iwapo muda huo utazidi, timu husika itapoteza umiliki wa mpira kwa wapinzani.

‎Katika suala la matibabu, mchezaji anayehudumiwa uwanjani atalazimika kutoka nje kwa muda wa dakika moja kabla ya kurejea kucheza, isipokuwa pale ambapo ameumia kufuatia faulo iliyostahili adhabu ya kadi.

‎Vilevile, mfumo wa usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR) sasa utaruhusiwa kupitia matukio ya kadi ya pili ya njano inayoweza kusababisha mchezaji kutolewa nje, pamoja na maamuzi ya kona yaliyotolewa kimakosa.

‎FIFA pia imesisitiza kuwa ni nahodha pekee atakayekuwa na ruhusa ya kumfuata mwamuzi kwa ajili ya maelezo, huku wachezaji wengine wakikabiliwa na adhabu ya kadi ya njano endapo watamzingira mwamuzi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments