Friday, December 12, 2025
spot_img
HomeHabariHii ndiyo Nyasa ya Dk. Samia

Hii ndiyo Nyasa ya Dk. Samia

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itakamilisha utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbambabay na kuukamilisha mapema mwakani, ili kutimiza ndoto ya wakazi wa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

Dk. Samia ameyasema hayo leo, Jumapili Septemba 21, 2025 alipowahutubia wananchi wa Mbambabay mkoani Ruvuma, katika mkutano wake wa kampeni za urais, ambazo kwa sasa zimeingia mikoa ya kusini.

Amesema ujenzi huo unafanyika, baada ya Serikali yake kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Ndumbi wilayani humo hivyo, na kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo kutoka tani 40,000 hadi 110,000 kwa mwaka, huku abiria wakihudumiwa 100,000 kutoka 45,000 kwa mwaka.

Sambamba na miradi hiyo, amesema katika Wilaya ya Nyasa kutatekelezwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) yenye urefu wa kilomita 1,000. Upembuzi yakinifu wa kwanza umekamilika na mipango imesharekebishwa ili kazi ianze.

“Itapita maeneo yenye utajiri wa mazao ya nafaka na kuunganisha maeneo ya kiuchumi ya Liganga na Mchuchuma yenye utajiri wa chuma na makaa ya mawe. Tupo kwenye mazungumzo ya kujenga reli hii yenye kiwango cha kisasa kutoka Mtwara hadi Mbambabay,” amesema Dk Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments