Himid Mao afurahia kurejea Azam FC

Kiungo mkabaji Himid Mao ameonyesha furaha kubwa kurejea Azam FC baada ya miaka saba tangu aondoke kwenda kucheza Misri.

Himid alionekana kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu 2018, akisema amefurahi kukutana tena na sura alizozizoea.

Azam pia imemrejesha kipa Aishi Manula baada ya miaka nane Simba.

Himid amesema timu iko chini ya kocha Florent Ibenge, na amewataka wachezaji wote kushirikiana kufanikisha malengo ya klabu.

Azam itaweka kambi Karatu kabla ya kuelekea Kigali kujiandaa na msimu mpya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *