Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeMichezoJKT Queens waanza kwa kishindo dhidi ya Bunda Queens

JKT Queens waanza kwa kishindo dhidi ya Bunda Queens

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake, JKT Queens, wameruhusu upepo wa ushindani kuanza leo wanapokutana na Bunda Queens kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Hii ni mechi ya kwanza kwa JKT Queens baada ya kurejea kutoka CECAFA, ambako walikuwa wakipeperusha bendera ya Afrika Mashariki na Kati kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire, amesema wachezaji wako tayari kuendeleza ushupavu wao kwa kila mpinzani watakayemkabili:

“Kila mechi kwetu ni fainali. Hatutegemei mchezo rahisi kwa sababu kila timu imejipanga.”

Kwa upande wa Bunda Queens, Kocha Alley Ibrahim, amesema watakosa wachezaji watano muhimu kutokana na kutokamilika kwa leseni zao.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa hawatakuwa kibarua rahisi:

“Tumepungukiwa, lakini tumejenga morali ya wachezaji waliopo. Tunaomba dua za mashabiki tupate pointi muhimu za kurejea kwenye ushindani.”

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments