Mbunge wa Jimbo la Nyasa, John Nchimbi, ameapishwa rasmi Novemba 11, 2025, Bungeni jijini Dodoma, kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2025 hadi 2030.
Hii ni mara ya kwanza kwa Nchimbi kula kiapo cha ubunge kwa Jimbo la Nyasa, baada ya kupata imani ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu.




