Friday, March 27, 2026
spot_img
HomeHabariKamati ya LAAC yatua Magu, yasisitiza miradi kukamilika kwa wakati

Kamati ya LAAC yatua Magu, yasisitiza miradi kukamilika kwa wakati

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya Mwenyekiti wake Ado Shaibu Ado imetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Shule ya Sekondari ya Magu.

Kamati imeiagiza Halmashauri ya Magu kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika ikiwemo kufanyia kazi dosari zilizobainika katika ujenzi. Kamati imesisitiza pia umuhimu wa Halmashauri kuzingatia taratibu za kisheria na kimkataba katika kuwasimamia wakandarasi.

“Ni lazima tuuvunje utaratibu wa kusubiri Kamati ya LAAC au viongozi waandamizi wa TAMISEMI waje ndio kazi dosari zionekane na kufanyiwa kazi. Wataalam katika Halmashauri wafanye kazi kwa weledi kuhakikisha kuwa wanasimamia viwango vinavyotakiwa kwenye ujenzi” alisisitiza  Ado


RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments