Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Juma Kaseja, amesema lengo lake ni kushinda michezo miwili ya mwanzo ya Ligi ya Championship itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Kagera Sugar itaanza Oktoba 10 dhidi ya Transit Camp kabla ya kuvaana na Berberian Oktoba 18.
Kaseja alisema ushindi wa pointi sita utawapa morali wachezaji, mashabiki na benchi la ufundi kuelekea safari ya kurejea Ligi Kuu.
Aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu yao akisisitiza maandalizi yamekamilika baada ya wiki tatu za kambi.





