Kocha wa KMKM, Hababuu Ali amesema anaboresha kikosi chake kuelekea mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Port ya Djibouti.
Licha ya kushinda 2-1 kwenye uwanja wa nyumbani, alisema wanahitaji kuongeza umakini hasa safu ya ushambuliaji na ulinzi.
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ameahidi kutoa Sh milioni tano kwa kila goli litakalofungwa na timu za Zanzibar kama motisha, ambapo KMKM tayari imejipatia Sh milioni 10.