Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeMichezoKocha Bares: Ushindani Mkali Waongeza Thamani ya Ligi Kuu Zanzibar

Kocha Bares: Ushindani Mkali Waongeza Thamani ya Ligi Kuu Zanzibar

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Zanzibar unakaribia kumalizika, na Kocha Mkuu wa Zimamoto, Abdallah Mohamed ‘Bares’, amesema ushindani wa msimu huu unaonesha kiwango cha soka la Zanzibar kupanda kwa kasi.

Amesema timu nyingi zimefanya maboresho ya vikosi kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu kutoka Bara na nje ya Visiwa hivyo:

“Miaka ya nyuma ligi haikuwa ngumu kiasi hiki. Kila timu imejipanga, kila mechi ni vita.”

Bares amesema kikosi chake cha Zimamoto kina ubora, lakini wanahitaji maboresho zaidi kwenye safu ya ushambuliaji ili kuongeza ufanisi.

Ligi Kuu Zanzibar humtoa mwakilishi wa CAF Champions League, huku ZFF Cup ikipeleka mwakilishi kwenye CAF Confederation Cup.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments