Baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kwa kuchapwa 4-1 na TP Mazembe, Kocha wa JKT Queens, Kessy Abdallah amesema wapinzani wao walikuwa bora zaidi na walifanya makosa ya kitoto yaliyosababisha mabao rahisi.
Alisema licha ya kutolewa, wamepata somo kubwa na wakipata nafasi tena mwakani watarejea wakiwa bora zaidi.
JKT Queens ilikuwa inahitaji ushindi ili kufuzu, lakini imehitimisha mashindano ikiwa nafasi ya tatu Kundi B kwa pointi mbili, na kuendelea kuishia hatua ya makundi kama ilivyokuwa 2023.
Asec Mimosas na TP Mazembe zimefuzu nusu fainali, huku upande wa Kundi A, AS FAR na Masar zikitinga hatua hiyo.





