Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka amesema kuteuliwa kwa Jaji mstaafu Profesa Ibrahim Juma kumetokana na uzoefu alionao katika tasnia ya sheria na utoaji haki.
Ameutaja wasifu wa Profesa Juma kuwa, amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 2017 hadi 2025 alipostaafu na kabla ya hapo alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya wadhifa huo, amesema alikuwa Jaji wa Makahama Kuu, akitokea kuwa Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katika utumishi wake, amesema amewahi kupata nishati ya Muungano Daraja la Pili na amekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.




