Bondia wa kulipwa, Mussa Makuka, amejigamba kuwa atamchapa mpinzani wake Ally Ngwando kwenye pambano lao litakalofanyika Desemba 26, Masaki jijini Dar es Salaam. Makuka alisema amejiandaa vya kutosha na ana uhakika wa ushindi.
“Ninafanya mazoezi makali kuhakikisha nakifanya nilichokusudia. Mpinzani wangu ajipange tu,” alisema.
Makuka aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya ngumi, akisisitiza kuwa hakuna kitakachomzuia kupata ushindi kutokana na maandalizi mazuri anayoyafanya.




