Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na Baraza la Waislamu Tanzania, (Bakwata), zimesema nitahakikisha zinailinda amani nchini kwa gharama yoyote, huku zikizisisitiza taasisi mbalimbali kuacha kutoa matamko yanayochochea chuki na uhasama kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa, Alhamisi Novemba 20, 2025 na Amiri wa Baraza Kuu na Jumuiya za Taasisi hizo, Sheikh Mussa Kundecha alipozungumza na wanahabari, jijini Dar es Salaam.
Ametaka zitumike kauli za kujenga na umoja na kuwa na mshikamano baina ya Waislamu, wasio Waislamu na Watanzania kwa ujumla.




