Monday, December 15, 2025
spot_img
HomeHabariMatatani madai kujiteka akitaka mume wake atoe milioni 10 asitolewe mimba

Matatani madai kujiteka akitaka mume wake atoe milioni 10 asitolewe mimba

Mwanamke Loveness Kisile (30), mkazi wa Mtaa Temeke, Kata ya Mhandu, Wilaya ya Nyamagana, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mwanza kwa kudanganya mumewe atoe shilingi milioni 10 ili asidungwe sumu ya kuondoa mimba ya mapacha watatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, alisema Loveness alidai kupitia simu kutekwa na watu watatu wa jinsia ya kiume waliomlazimisha kulipa fedha, na kwamba watoto wake mapacha wamefariki.

Tuhuma hizi zilisababisha taharuki kwa mume wake na jamii kwa ujumla.

Polisi walimkamata salama akiwa amejificha katika Mtaa wa Mecco, Kata ya Buzuruga, Wilaya ya Ilemela. Baada ya kufanyiwa vipimo vya kitabibu, ilithibitishwa kuwa hakuwahi kupata ujauzito na alikiri kudanganya ili kumshawishi mumewe.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments