Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariMatuluma ashinda umeya kwa kura 27 kati 28 zilizopigwa

Matuluma ashinda umeya kwa kura 27 kati 28 zilizopigwa


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kahaka mkoani Shinyanga, limempitisha Diwani wa kata ya Nyasubi, Matuluma Kaniki kuwa Mwenyekiti wa Manispaa hiyo kwa kupata kura 27 kati ya kura 28 zilizopigwa leo.

Akizungumza baada ya kupitishwa Kaniki alisema atahakikisha anashiriliana na madiwani wake kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo hasa kupitoa sera walizokuwa wakizinadi katika kampeninza uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Alisema, atahakikiaha vijana wapata mikopo iliyopo kisheria ili kihakikisha wanajiinua kiuchumi na kuondokana na utegemezi, kwani kila mwaka Maniapaa imekuwa ikitenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine: Baraza hilo limemchagua Shabani  Mikokongoti, diwani wa kata ya Mwendakulima kuwa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo huku nae akiahidi kumsaidia Mwenyekiti katika utekelezaji na kuwahudumia wananchi.

Aidha kikao hicho pia kiliambatana na uapisho ikiwa ni hatua rasmi ya kuwawezesha kuanza kutekeleza majukumu yao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Manispaa hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments