Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariMatumizi ya nishati safi ya kupikia yaongezeka nchiniĀ 

Matumizi ya nishati safi ya kupikia yaongezeka nchiniĀ 


šŸ“Œ Mhandisi Mramba asema yamefikia asilimia 20.3Ā  kutoka asilimia 6.9 ya mwaka 2021

šŸ“Œ Lengo ni kufikia asilimia 80 ifikapo 2034

šŸ“Œ Apongeza juhudi za Rais Samia katika kuwezesha upatikanaji wa nishati safi, salama na nafuu kwa Watanzania

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha.Felchesmi Mramba ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchinj yameongezeka kutoka asilimiaĀ  6.9 mwaka 2021 hadi asilimiaĀ 20.3 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 80 ndani ya miaka 10, ambapo hadi sasa imebakia miaka 9.

Mha. Mramba ameyasema hayo Septemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kongamano laĀ  Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi kwa ushirikianoĀ  na Wizara ya Nishati pamoja na wadau mbalimbali likibebwa na kaulimbiu yaĀ  ā€˜Nishati safi ya Kupikia Okoa Maisha, Linda Mazingira.

AkizungumzaĀ  wakati wa uzinduzi huo, Mha. Mramba amesemaĀ  ā€œNishati Safi ya Kupikia siyo jambo la kinadharia bali ni jambo linalohusu maisha, mazingira na uchumi huku msingi wake mkuu ukiwa ni kulinda afya, mazingira pamoja na maendeleo jumuishi.ā€Ā 

Aidha, Mhandisi Mramba ameendelea kuwahamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia akikumbusha kuwa, takwimu zinaonesha kuwa takribani watanzania 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uvutaji wa moshi unaotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo kuni na mkaa.

Ameeleza kuwa kutokana na athari hizoĀ  Ā SerikaliĀ chini yaĀ uongoziĀ wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,Ā  imeandaaĀ Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034Ā uliozinduliwa mwezi Mei 2024 ambao utawezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia.

Sanjari na hayo, Mha. Mramba amemshukuru Rais,Ā  Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye niĀ kinara wa nishati safi ya kupikia kitaifa na kimataifa kwa Uongozi wake wa mfano na dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha kila Mtanzania anatumia nishati safi, salama na nafuu ya kupikia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments