Mbeya City yawapa nafasi Mtibwa, Geita yakwama

Mbeya City imezidi kuwaweka Mtibwa Sugar kwenye nafasi nzuri ya kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Geita Gold 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Championship uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao pekee la Kilaza Mazoea dakika ya 62 limeipandisha Mbeya City hadi nafasi ya nne na kufikisha pointi 25.

Geita Gold, ambayo iko nafasi ya pili kwa pointi 27, bado inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa vinara wa ligi, Mtibwa Sugar, waliozidi kuimarisha uongozi wao baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bigman FC, bao likifungwa na Juma Luizio dakika ya 52.

Ushindi huo unaipa Mtibwa tofauti ya pointi tano na matumaini makubwa ya kupanda moja kwa moja.

Biashara United pia iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Green Warriors, huku Polisi Tanzania ikiichapa Songea United 1-0, zikijipatia nafasi za kati kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16.

Timu mbili za juu zitapanda moja kwa moja Ligi Kuu, huku nafasi ya tatu na nne zikicheza mechi za mchujo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *