Mchungaji apongeza mfanyabiashara Said Lugumi kwa kuwajengea yatima maghorofa

Mchungaji wa Kanisa la Miracle International, Daniel, akiwa katika madhabahu ya kanisa hilo, amempongeza na kumtolea mfano mfanyabiashara Said Lugumi kwa kuwajengea watoto yatima maghorofa matano kwa ajili ya makazi na kuwalea kama watoto wake wa kuwazaa.

Mchungaji Daniel ametolea mfano huo mbele ya waumini wake, akisisitiza umuhimu wa kutenda mema kwa wengine pasipo kujali imani zao za kidini. “Huyu Said Lugumi ameishia darasa la saba, lakini amewajengea yatima maghorofa matano. Kila ghorofa lina uwezo wa kuishi yatima 100.

Je, huyu mtu hatapata thawabu kutoka kwa Mungu ambaye anawaangalia yatima? Atapata, kwa sababu amewaangalia wale wasiokuwa na uwezo,” alisema Mchungaji Daniel.

Aliongeza, “Yule Lugumi si Muislamu, lakini amewatendea yatima mema. Kama dini yako haikuzuii kutenda mabaya na inakuacha unatenda mabaya, lakini dini ya mwingine inamruhusu kutenda mema, dini iliyo njema ni ipi? Si ni kutendea watu mema?”

Mchungaji Daniel pia alieleza kuwa Lugumi si tu amewajengea yatima makazi, bali pia hualika watoto hao kila mwaka kwa sherehe na kula pamoja nao.

“Yeye anawatendea mema wale ambao hata si ndugu zake. Fanyeni mema kama maandiko yanavyosema: ‘Tusichoke kutenda mema maana katika kutenda mema hatutazimia mioyo.’”

Alihitimisha kwa kusema, “Lugumi anawalisha watu ambao wazazi wao walikuwa na maisha tofauti, lakini yeye amefika mahali pa kuwajengea maghorofa matano. Unafikiri wale yatima wanapomuangalia, wanamwambia Mungu: ‘Tunashukuru.’ Si sifa zinarudi kwa Mungu? Mungu naye anasema: ‘Lugumi, uko wapi? Njoo nikuongezee kingine.’”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *