Mfanyabiashara mdogo maarufu Machinga jijini Dar es Salaam, Linton Mussa amesema tishio la vurugu Dessemba 9, 2025 limekwamisha kipato chake cha siku, huku akiwasihi vijana kuidumisha amani.
Amesema mlo wake wa siku unategemea mauzo ya biashara yake na jana alikosa wateja kutokana na wengi kukaa nyumbani kwa hofu ya kuwepo kwa vurugu.
Amesisitiza umuhimu wa amani, akiwasihi vijana kuhakikisha wanaidumisha ili kuwepo uhuru wa kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii.




