Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeHabariMiaka 64 ya uhuru, Watanzania wamechagua amani

Miaka 64 ya uhuru, Watanzania wamechagua amani

Maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru yamefanyika kipekee, yameadhimishwa kwa namna yake, si tu yameacha funzo, bali yameonyesha jinsi Watanzania wanavyothamini tunu muhimu za amani, umoja na mshikamano.

Ukimya na utulivu uliogubika taifa Desemba 09, haukuwa na maana nyingine isipokuwa fursa ya watanzania kutafakari maana na thamani ya uhuru wao, zaidi sana thamani ya amani na mshikamano ambavyo vimekuwa utambulisho wetu kama taifa mbele ya dunia.

Katika tafakuri hiyo bila shaka kila mtanzania amepata fursa ya kuidurusu walau kwa ufupi safari ya miaka 64 ya Tanzania huru, kwanini Tanzania imeendelea kuwa Tanzania, yaani Taifa – na siyo pande kubwa la ardhi lenye mipaka ya kijiografia ambalo linakaliwa na watu zaidi ya milioni sitini.

Tanzania Ilishafuzu (graduate) kutoka kuwa lijipande kubwa la ardhi ambalo watu wake walipata uhuru kutoka kwa Waingereza hadi kuwa taifa ambalo watu wake wanaishi kwa umoja, amani na mshikamano, ambamo thamani ya mtu inapimwa kwa utu wake. Watanzania kuitana majina kwa kutanguliza neno ndugu hata kama siyo ndugu yako wa damu haikuwa bahati mbaya, huo ulikuwa msingi wa taifa ambalo watu wote wanathaminiana kama ndugu.

Kimya cha Desemba 09, kimewapata fursa watanzania kutathmini na kuijua maana halisi ya amani na mashikamano wao, waswahili wanasema, unapokuwa na kitu unaweza usijue thamani yake, lakini kitapapokosena ndiyo utajua thamani yake halisi (You can’t miss what you have until you lose it). Baada ya kuonja kidogo tu hali inayofanana na kukosekana kwa amani na utulivu sasa wanajua thamani yake halisi.

Ndiyo maana baada ya tafakuri ya kimya cha Desemba 09, kila mtu ameamua kukataa kuingia tena kwenye mtego wa kutaka kuvuruga amani, umoja na mashikamano wetu. Ukiongea na watu, ukiwatazama nyuso zao, ukiangalia mienendo yao yote ina ujumbe mmoja tu – Baada ya tafakuri ya Desemba 09 wamechagua AMANI.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments