Mkazi wa Shinyanga, Mbole John amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kudhibiti tishio la vurugu Desemba 9, mwaka huu, akisema machafuko hayachagui nani wa kumwathiri.
Amesema iwapo vyombo hivyo visingedhibiti pengine yangetokea kama ya Oktoba 29 na kuyaathiri makundi yote ya wananchi na shughuli za kiuchumi.
Ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani, kwa kuwa ndio inayofanya watu wanaishi kwa urafiki, kindugu na kuwa huru kufanya shughuli zao.




