Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeMichezoMnyama aangushwa Mkapa – Azam yamaliza usongo kwa Simba 2-0

Mnyama aangushwa Mkapa – Azam yamaliza usongo kwa Simba 2-0

Azam FC jana ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya sare tatu mfululizo kwa kuichapa Simba SC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ushindi uliotokana na mabao ya Jephte Kitambala Bola na Idd Selemani ‘Nado’.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu huu baada ya kushinda michezo minne ya mwanzo.

Mabao yote yalifungwa dakika 10 za mwisho, huku mchezaji aliyeingia kipindi cha pili, Nassor Saadun, akiibuka kinara wa usumbufu uliowapa Azam mabao yote mawili.

Bao la kwanza lilitokana na shambulio la kujibu dakika ya 81, Saadun akatoka kasi wingi ya kushoto na kumpa pasi Kitambala Bola aliyekwamisha mpira wavuni. Dakika saba baadaye, Saadun tena aliingia ndani ya boksi na kutengeneza pasi iliyomkuta Nado aliyehitimisha bao la pili.

Azam sasa ina pointi tisa kwenye msimamo baada ya michezo mitano.

Simba yajilaumu

Licha ya kupoteza, Simba ilisimamia kipindi cha kwanza lakini ikapoteza nafasi nyingi muhimu ambazo zingebadili matokeo.

Mukwala, Mpanzu na Mutale walipata nafasi za wazi—ikiwemo mpira kugonga nguzo na makosa ya umaliziaji yaliyowagharimu.

Kitambala Bola naye alipoteza nafasi ya wazi dakika ya 28 kwa upande wa Azam, huku kipindi cha pili Mpanzu akigonga mwamba sekunde za mwanzo tu.

Kwa matokeo hayo, Simba inabaki na pointi 12 baada ya mechi tano.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments