Saturday, March 21, 2026
spot_img
HomeMichezoMshtuko AFCON: Yadaiwa Osimhen ameondoka kambi ya Super Eagles

Mshtuko AFCON: Yadaiwa Osimhen ameondoka kambi ya Super Eagles

Ripoti zilizothibitishwa zinaeleza kuwa mshambuliaji nyota wa Nigeria, Victor Osimhen, ametangaza rasmi kujiondoa katika timu ya taifa ya Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Osimhen aliacha kitambulisho chake cha mashindano (accreditation) na kudai kuwa anarudi nchini Uturuki, hatua iliyotafsiriwa kama kumaliza kabisa ushiriki wake na kikosi cha Super Eagles.

Taarifa hiyo imeripotiwa na OneJoblessBoy, kupitia mtangazaji wa Arise TV, Aron Akerejola.

Uamuzi huo umeibua mshtuko mkubwa ndani ya kambi ya timu ya taifa ya Nigeria pamoja na miongoni mwa mashabiki wa soka barani Afrika, hasa ikizingatiwa kuwa Nigeria ipo katikati ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Hadi sasa, Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) halijatoa tamko rasmi kueleza au kufafanua tukio hilo, hali inayozidi kuongeza sintofahamu kuhusu mustakabali wa Super Eagles katika mashindano hayo yanayoendelea.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments