Mtume Mwaposa ampa kongole Lugumi kusaida wenye uhitaji

Mtume Boniface Mwamposa ‘Buldoza’ wa Kanisa la Inuka Uangaze amempongeza mfanyabiashara, Said Lugumi kwa kujenga maghorofa matano kwa ajili ya watoto yatima.

“Nampongeza (Lugumi) niliona kwenye mitandao, hatakiwi kuvunjwa moyo, ni jambo jema limefanyika, ndani yake kuna roho ya kumcha Mungu,” amesema Mwamposa.

Zaidi ya watoto 800 wenye mahitaji maalumu na wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam watanufaika na majengo hayo yanayotarajiwa kukamilika Machi, mwaka huu.

Awali jengo moja la ghorofa nne lililopo Mtaa wa Msufini, Mwananyamala lilikabidhiwa Desemba 25, mwaka jana kwa watoto hao wakati wa hafla ya chakula kilichoandaliwa na Lugumi kwa ajili ya watoto hao.

Majengo hayo yatahudumia watoto zaidi ya 800 na kila jengo lina uwezo wa kuchukua zaidi ya watoto 100.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *