Tuesday, December 9, 2025
spot_img
HomeMichezoMukwala kuelekea Raja Casablanca, Simba yatafuta mbadala

Mukwala kuelekea Raja Casablanca, Simba yatafuta mbadala

Straika wa Simba SC, Steven Mukwala, yuko mbioni kutua Raja Casablanca ya Morocco katika dirisha dogo la usajili, ambapo ataungana na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Fadlu Davies, ambaye sasa ni kocha mkuu wa timu hiyo.

Simba SC imekubali kumuachia Mukwala kutokana na mipango mipya ya kikosi hicho, ikiwemo kuwa na machaguo mengine kama Jonathan Sowah na Seleman Mwalimu, ambao wanaonekana kuendana na falsafa mpya ya benchi la ufundi. Klabu hiyo inapanga kusajili mshambuliaji mwingine kujaza nafasi ya Mukwala.

Chanzo kinasema kuwa kiwango cha Mukwala kimeshuka, hasa katika upande wa ufungaji, hali iliyochangia kushuka kwa morali yake ndani ya Simba.

Zaidi ya hapo, taarifa zinaeleza kuwa kuna kiungo mwingine wa Simba anayetajwa pia kutua Raja Casablanca baada ya meneja wa usajili wa klabu hiyo, Pantev, kumkataa awali — na jina litatajwa baadaye kadri mchakato unavyokamilika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments