Wednesday, December 17, 2025
spot_img
HomeHabariNchimbi- Serikali kutenga hekta 20,000 kwa wakulima nyasi za mifugo Njombe

Nchimbi- Serikali kutenga hekta 20,000 kwa wakulima nyasi za mifugo Njombe

Kampeni za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikizidi kushika kasi, Mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa Serikali ijayo ya CCM ikiongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan itatenga hekta zaidi ya Elfu Ishirini kwa ajili ya Wakulima wa Nyasi za Mifugo.

Dk. Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 23, 2025 akiwa Wilayani Makete, Njombe ikiwa Muendelezo wa Mikutano ya Kampeni za Urais kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nilikuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Nyasi Maarufu za Ng’ombe kule zinaitwa Nyasi za Tanzania, wakati sisi hapa wenyewe hatuzijui, kwa hiyo mkakati Ujao wa Serikali ni Kutenga zaidi ya Hekta elfu Ishirini kwa ajili Wakulima wa Nyasi za Mifugo na hapa Makete mnaongoza kwa hilo” amesema Dk.Nchimbi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments