Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariNiffer, Mika Chavala wafutiwa kesi ya uhani iliyokuwa ikiwakabili

Niffer, Mika Chavala wafutiwa kesi ya uhani iliyokuwa ikiwakabili

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin (26) maarufu Niffer na Mika Lucas Chavala, waliokuwa na kesi ya uhaini.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 03, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada wakili wa Serikali, Titus Aron kuileleza Mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao wawili.

DPP amewafutia kesi hiyo namba 26388/ 2025 chini ya kifungu namba 92(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 20 ilivyofanya marejeo mwaka 2023.

“Mahakama inakubaliana na ombi la upande wa Jamhuri kama lilivyowasilishwa, hivyo inawaachia huru washtakiwa hawa wawili,” amesema Hakimu Lyamuya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments