Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya, Septemba 26, 2025, amepokea vifaa tiba vilivyotolewa na Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii.
Vifaa hivyo vinavyotarajiwa kuboresha huduma za afya ni pamoja na vitanda 20 vya wanawake kujifungulia, vitanda 20 vya uchunguzi pamoja na mashine 20 za kusaidia kupumulia kwa watoto wachanga wenye changamoto za kiafya.




Akizungumza katika makabidhiano hayo, DC Mikaya ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba, sambamba na kuiunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha sekta ya afya kupitia ujenzi wa hospitali mpya.


“NMB wameonyesha mfano bora wa mshirika wa maendeleo kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. Vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Kigamboni,” amesema DC Mikaya.





