Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeBiasharaParachichi za Tanzania kupata ubora mpya, aina tano zasajiliwa rasmi na TOSCI

Parachichi za Tanzania kupata ubora mpya, aina tano zasajiliwa rasmi na TOSCI

Wakulima wa parachichi nchini wamepata nafuu baada ya Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kutangaza usajili wa aina tano bora za miche ya zao hilo, hatua inayolenga kuongeza thamani na ushindani wa Tanzania katika soko la kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Nyasebwa Chimagu, alisema aina hizo ni Hass, Fuete, Pikatoni, Xikulu na Booth7, ambazo zinatajwa kustahimili magonjwa na kutoa mazao yenye kiwango bora kwa biashara.

Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya tatu barani Afrika kwa uzalishaji wa parachichi, baada ya Afrika Kusini na Kenya, huku uzalishaji ukikadiriwa kufikia tani 198,000 kwa mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Nyasebwa Chimagu akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya taasisi hiyo kuhusu usajili wa mbegu.

“Tunataka miche bora na iliyothibitishwa iwe msingi wa wakulima wetu ili kuongeza tija na kuiweka Tanzania kileleni mwa uzalishaji wa parachichi Afrika,” alisema Chimagu.

Aidha, TOSCI imetoa wito kwa wazalishaji wote wa miche kujisajili mapema ili kupata uhalali wa kisheria na kushiriki kikamilifu kwenye soko la kimataifa, huku baadhi ya waliokwisha sajiliwa wakieleza kuwa hatua hiyo imewapa nafasi ya kuongeza mapato na kupanua biashara zao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments