Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeHabariPEDIMA azidi kung'ara kwa mageuzi, ubunifu sekta ya kidijitali, ahamasisha vijana

PEDIMA azidi kung’ara kwa mageuzi, ubunifu sekta ya kidijitali, ahamasisha vijana

Mfanyabiashara chipukizi, Peter Didas Mallya maarufu kama PEDIMA, ameendelea kuibua mvuto mkubwa katika tasnia ya biashara nchini kutokana mchango wake katika sekta za kifedha, teknolojia, afya na ajira kwa vijana kutumia teknolojia ya kidijitali ambazo zimechagia apate tuzo zaidi ya tano.

Kupitia kampuni zake, mfanyabiashara huyo chipukizi, amejiimarisha kama mmoja wa vijana wanaoongoza mageuzi ya kidijitali na kutoa huduma bunifu zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Akizungumzia safari yake ya ujasiriamali na maono yake kwa taifa, PEDIMA amesema anaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini.

“Ninaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa. Lengo langu ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira, na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini,” amesema.

Ameeleza kuwa kampuni zake zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika jamii kupitia ubunifu unaolenga kutoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali za wananchi. 

“PEDIMA Enterprises inatoa huduma za super-agency na mobile money aggregation ikiwawezesha mawakala na wafanyabiashara kufanya miamala kwa urahisi zaidi,” amesema.

Akifafanua kuhusu PEDIMA Microfinance, amesema taasisi hiyo imekuwa nguzo muhimu kwa vijana na wafanyabiashara wadogo kupitia mikopo nafuu na elimu ya ujasiriamali.

Kadhalika, amesema kupitia kampuni zake, pia wamekuwa wakibuni mifumo ya malipo ya kidijitali na huduma za kifedha mtandaoni, hatua inayoongeza ushirikishwaji wa kifedha nchini. 

Huduma nyingine ambazo zinatolewa na kampuni hizo, ni kutengenza pia bidhaa za afya. 

Amesema kupitia kazi zake hizo, amefanikiwa kupata tuzo mbalimbali zaidi ya tano na akawahamasusha vijana wenzake wasikate tamaa ya kufanya kazi na kujituma kuanzisha kampuni ili kuendelea kutengeneza ajira na kupanua uchumi wa kundi hilo na kuziba pengo la ukosefu wa ajira.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments