Tuesday, March 24, 2026
spot_img
HomeBiasharaProf. Mkumbo aimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Prof. Mkumbo aimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Biashara wa Jimbo la Shandong, Wang Lei, ambapo wamejadili masuala ya kimkakati na namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuhamasisha uwekezaji kati ya Tanzania na Jimbo la Shandong nchini China, hususan katika sekta muhimu za maendeleo.

Katika kikao hicho, Prof. Mkumbo aliridhia mapendekezo na makubaliano yaliyowasilishwa, yakiwemo ya kuanzisha na kuimarisha ushirikiano katika sekta za viwanda, madini, kilimo na utalii.

Mbali na kikao hicho, Prof. Mkumbo pia alifanya mazungumzo ya kina na wawekezaji mbalimbali wanaotarajia kuwekeza nchini Tanzania.

Miongoni mwa wawekezaji hao ni kampuni ya Anhui Conch Cement Co., Ltd, inayojihusisha na uzalishaji wa saruji, iliyowakilishwa na Terry Chu. Kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania, ikiwa ni hatua yao ya kwanza kuingia katika soko la Afrika.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada endelevu za serikali za kuvutia uwekezaji wa kimataifa kupitia makongamano na vikao vya kimkakati vinavyolenga kukuza na kuendeleza sekta ya uwekezaji nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments