Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariPSSSF yawajengea uelewa waandishi wa habari Tabora

PSSSF yawajengea uelewa waandishi wa habari Tabora

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewajengea uelewa waandishi wa habari mkoani Tabora kwa lenbo la kujua shughuli zinazotekekelezwa na Mfuko huo ili waweze kuripoti vema masuala yahusuyo hifadhi ya Jamii.

Katika kikao kazi kilichofanyika mjini Tabora, chini ya uratibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Tabora (TPC) ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Juma Kapipi aliishukuru PSSSF kwa kuandaa kikao hicho muhimu kwa waandishi wa habari mkoani humo.

“Kwa kweli TPC tumefarijika kwa PSSSF kutuletea mafunzo hayo muhimu, nina imani kuanzia sasa waandishi wetu watakuwa wanaandika habari za PSSSF kwa ufasaha, tunaomba mafunzo hayo yawe mlango wa kufungua ushirikiano chanya kwa pande zote” alifafanua Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa bodi ya Umoja wa Klabu za uandishi wa habari Tanzania (UTPC) Salma Abdul alisisitiza ili PSSSF iweze kufanikiwa kwenye utendaji kazi lazima kuwepo na ushirikiano bora na waandishi wa habari, ili inapotokea changamoto kwa wananchi waandishi waweze kupata ushirikianao thabiti kwa kujibu masuala yahusuyo huduma na kuandika habari sahihi badala ya kuruhusu uvumi.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo Pendo Sallu ambaye ni mwanachama wa TPC ameishukuru PSSSF kwa semina hiyo na kuwahakikishi kuwa watakwenda kuandika habari mbalimbali za kuelimisha na kuisaidia jamii juu ya masuala ya hifadhi ya jamii.

“Kwanza tunawashukuru PSSSF kwa semina hii, Tunawahakikishia kuwa tutakwenda kuandika habari mbalimbali za kuelimisha na kuisaidia jamii, Tunawaomba watumishi kutoka PSSSF wadumishe mawasiliano na ushirikiano hasa tunapokuwa tunataka ufafanuzi” alishauri Pendo Sallu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Uhusiano wa PSSSF Abdul Njaidi, amesisitiza wajibu wa waandishi wa habari kuandaa vipindi na makala zinazotoa elimu ya kina kuhusu kinga ya jamii, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia wananchi kuondokana na malalamiko yanayotokana na ukosefu wa taarifa, na badala yake wataelewe vizuri sera, kanuni, mafao na faida tele zinazotolewa na Mfuko.

Ushirikiano kati ya PSSSF na waandishi wa habari wa Tabora unatarajiwa kuimarisha uwazi na kuleta matokeo chanya katika kufikisha taarifa sahihi kwa Watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla kwa kuondoa malalamiko na kujenga imani katika Mfuko.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments