Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariPutin ampongeza Dk. Samia kushinda Urais

Putin ampongeza Dk. Samia kushinda Urais

Rais wa Urusi, Vladmir Putin ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Katika uchaguzi huo, Dk. Samia amefanikiwa kutetea nafasi hiyo, baada ya kupata ushindi wa kishindo wa kura milioni 31.913,866 sawa na asilimia 97.66 kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, leo Alhamisi Novemba 6, 2025 Rais Putin ametuma salamu za pongezi kwa Rais Samia kupitia ujumbe maalumu uliowasili Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments