Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariRais Samia arekebisha wizara mbili, aunda ya vijana

Rais Samia arekebisha wizara mbili, aunda ya vijana

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza baraza jipya la mawaziri, likihusisha wizara 27, huku akitimiza ahadi yake ya kuunda wizara kamili ya vijana.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, wizara hiyo itakuwa chini ya ofisi yake na itaitwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana na kwamba Joel Nanauka ameteuliwa kuiongoza.

Rais Samia ametangaza baraza hilo leo, Jumatatu Novemba 17, 2025 katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Sambamba na wizara hiyo, pia amefanya marekebisho madogo na kuunda Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano.

“Atakayeshika nafasi hiyo atakuwa na kazi ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali kuhakikisha mahusiano mazuri,” amesema.

Aidha, marekebisho mengine yameshuhudiwa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na sasa imehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments