Rais Samia atunukiwa tuzo ya The Gates Goalkeepers Award mafanikio sekta ya afya

Rais Samia Suluhu Hassan leo, Februari 4, 2025, ametunukiwa tuzo ya The Gates Goalkeepers Award kutokana na mafanikio makubwa ya uongozi wake, hususan katika sekta ya afya.

Ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya 2022 imeonyesha kupungua kwa vifo vya uzazi kwa asilimia 80 pamoja na vifo vya watoto wachanga.

Tuzo hiyo imetolewa na The Gates Foundation jijini Dar es Salaam, na Rais Samia amekuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kuipokea, ikiwa ni uthibitisho wa utendaji wake bora unaotambuliwa kimataifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *