Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariRC Chalamila azuia mabaunsa, atuliza mgogoro wa nyumba Mikocheni

RC Chalamila azuia mabaunsa, atuliza mgogoro wa nyumba Mikocheni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemtembelea mjane Alice Haule kufuatia madai ya kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi Mikocheni, inayodaiwa kuwa sehemu ya urithi kutoka kwa marehemu mumewe, Justice Rugaibula.

Chalamila alisema kitendo cha kumtoa mtu kwa nguvu na kutumia mabaunsa ni udhalilishaji na hakitavumiliwa, akipiga marufuku matumizi ya mabaunsa kwenye migogoro ya nyumba na ardhi, akisisitiza kuwa ni jukumu la polisi kushughulikia masuala hayo.

Alice anadai alinunua nyumba hiyo mwaka 2007 na mumewe, lakini baada ya kifo chake mwaka 2022 alianza kudaiwa na mfanyabiashara Mohamed Yusuph, ambaye anasema alinunua nyumba hiyo kutoka kwa marehemu mwaka 2011 kwa Sh milioni 160.

Wakati Alice akilalamika hakupewa taarifa wala kushirikishwa kwenye mauziano hayo, upande wa Mohamed unadai ulinunua kihalali na nyaraka zote zipo, huku akitaka fidia ya Sh milioni 500 ili mgogoro huo umalizike.

Maafisa wa ardhi na polisi wamesema uchunguzi wa nyaraka unaendelea na hatua zitachukuliwa kwa wote waliohusika kwenye uvamizi huo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments