Kipa wa zamani wa Simba, Ally Salim, ameanza mazoezi rasmi na Dodoma Jiji FC, akipokewa kwa shangwe na wachezaji wenzake.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Moses Mpunga, alisema ujio wa Salim umeongeza hamasa kikosini kutokana na uzoefu wake wa kucheza Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa Simba.
Dodoma Jiji, iliyo chini ya Kocha Vicent Mashami, itafungua msimu wa Ligi Kuu Septemba 17 dhidi ya KMC.
Klabu hiyo imefanya usajili mkubwa ikiwemo Andy Bikoko (Tabora United), Castor Mhagama na Faraji Kayanda (KenGold), Miraji Ahumani (Coastal Union) na Edgar William (Fountain Gate).




