Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeBiasharaSamia kufufua viwanda vya korosho vilivyokufa Tunduru

Samia kufufua viwanda vya korosho vilivyokufa Tunduru

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake imepanga kuvifufua viwanda vyote vya kubangua korosho vilivyobinafsishwa na sasa havifanyi kazi.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumatatu Septemba 22, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni, uliofanyika katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, ukihudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika ahadi hiyo, amesema atahakikisha anafufua viwanda vya kubangua korosho vilivyobinafsishwa na sasa havifanyi kazi, ili kuhakikisha vinaendelea na kazi.

Kwa sababu hiyo, amesema ndiyo maana Serikali imepeleka umeme zaidi ya mahitaji ya wananchi wilayani humo, ili ukakidhi mahitaji ya viwanda hivyo na vile vitakavyojengwa kama sehemu ya mpango wa kila wilaya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments