Thursday, March 12, 2026
spot_img
HomeHabariSamia: Tutalifanyia kazi ombi la Makambako kuwa Wilaya

Samia: Tutalifanyia kazi ombi la Makambako kuwa Wilaya

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema ombi la Makambako kuwa Wilaya lililotolea na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga, analichanganya na maombi mengine ya halmashauri aliyoyapokea kutoka maeneo mbalimbali aliyotembelea.

Ameeleza kwa muda mrefu Serikali ilizuia kufungua maeneo ya utawala ili kupunguza gharama za uendeshaji. Kwa sababu maombi yamekuwa mengi, katika awamu ijayo ataangalia wapi panastahili.

“Ni hoja tutakayoizingatia wakati tunapanga maeneo ya utawala. Kwa hiyo niseme maombi yote tumeyachukua na tutayafanyia kazi,” amesema Dkt Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments