Friday, March 13, 2026
spot_img
HomeAfyaDk. Samia aweka msisitizo huduma zinazowagusa Watanzania

Dk. Samia aweka msisitizo huduma zinazowagusa Watanzania

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema atakapochaguliwa kuwaongoza Watanzania kwa awamu nyingine, ataendelea kutoa huduma zinazowagusa watu moja kwa moja.

Amesema huduma kama elimu, afya, maji na umeme hazitakuwa na mjadala, hadi kuhakikisha kila Mtanzania anaguswa nazo.

Dk. Samia ameyasema hayo leo, Jumamosi Septemba 6, 2025 alipozungumza na wananchi wa Mufindi mkoani Iringa, katika mwendelezo wa ziara zake za kampeni za urais.

“Kila mtoto wa Tanzania awe anakwenda shule na kama mnavyojua elimu yetu ni bila ada tutakwenda kwa mwendo huo huo, darasa la kwanza hadi kidato cha sit ana anapokwenda chuo kikuu anakuta mkopo unamsubiri,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments