Tuesday, March 24, 2026
spot_img
HomeMichezoSenegal yang’ang’ania Kombe la AFCON

Senegal yang’ang’ania Kombe la AFCON

Wakati Senegal ikijiandaa kuwasilisha rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kupinga kupokwa ubingwa wa AFCON 2025, taifa hilo linaendelea kujivunia kombe walilokabidhiwa baada ya ushindi dhidi ya Morocco.

Mapema leo, Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ameweka picha mpya ya wasifu wake (profile) ikiwa na kombe hilo, hatua inayoonyesha msimamo wa nchi hiyo juu ya ushindi huo.

Sambamba na hilo, Shirikisho la Soka Senegal (FSF) pia limechapisha picha ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa, maarufu kama Simba wa Teranga, Pape Thiaw, akiwa amelibeba kombe hilo.

Aidha, FSF imesisitiza kuwa haitarejesha kombe hilo hadi pale uamuzi wa rufaa yao utakapofanywa na CAS, huku wakiamini kuwa haki itatendeka kupitia mchakato huo wa kisheria.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments