Kocha wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi, amesema hali ya jua kali mchana ndiyo imepunguza kasi na ubunifu wa wachezaji wake, hali iliyowafanya washinde bao 1-0 pekee dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa KMC Complex.
Bao hilo pekee lilifungwa na straika Elvis Rupia dakika za nyongeza kipindi cha kwanza, likiwa la pili kwake msimu huu.
Gamondi alisema kama mchezo ungechezwa jioni, wangeweza kupata ushindi mnono zaidi.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars imefikisha pointi sita baada ya kushinda michezo miwili mfululizo.
Kocha wa Mashujaa, Salum Mayanga, alisema watajipanga upya kwa mechi yao inayofuata dhidi ya Pamba Jiji Oktoba 17.






