Friday, March 27, 2026
spot_img
HomeHabariTanzania yapongezwa  juhudi  mabadiliko nishati Mkutano wa ZIMEC 2026

Tanzania yapongezwa  juhudi  mabadiliko nishati Mkutano wa ZIMEC 2026


Rais wa Jamhuri ya Zambia, Hakainde Hichilema, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi anazozifanya katika kutekeleza ajenda ya mabadiliko ya nishati barani Afrika.

Pongezi hizo zilitolewa Machi 26, 2026 wakati wa kufunga mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati, Zambia International Mining and Energy Conference, uliofanyika kwa siku mbili nchini Zambia.

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Hichilema alisema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia, mkakati ambao umepata msukumo mkubwa chini ya uongozi wa Rais Samia.

Aidha, alibainisha kuwa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, Tanzania inaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Zambia kupitia sera rafiki pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayounganisha nchi za kanda hiyo.

Mbali na hilo, Dkt. Hichilema aliipongeza wizara ya migodi na maendeleo ya madini ya Zambia kwa kuweka lengo la kuzalisha tani milioni tatu za shaba ifikapo mwaka 2030, hatua inayotarajiwa kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa nchi hiyo.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini wa Tanzania, Steven Kiruswa, alipata fursa ya kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuimarisha shoroba za miundombinu ya kikanda ili kuongeza tija na ushindani wa kibiashara.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments