Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeufungia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora baada ya kugundua haukidhi vigezo vya kanuni za leseni za klabu.
Hii inamaanisha TRA United, iliyocheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji na kutoka sare ya 2-2, italazimika kutumia uwanja mwingine kwa michezo yake ya nyumbani hadi marekebisho yatakapokamilika.