Klabu ya TRA United imewataka mashabiki wake kuwa na subira baada ya kutoshinda mchezo wowote katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu.
Ofisa Habari, Christina Mwagala alisema timu bado inajitafuta na matokeo si mabaya ukizingatia wamecheza mechi chache kuliko timu nyingine.
TRA United imetoa sare tatu—2-2 dhidi ya Dodoma City na sare tasa mbili dhidi ya Pamba Jiji na Mashujaa FC.
Mwagala amewataka mashabiki kuwapa muda, akisema safari ya ushindi wataianza Novemba 22 watakapoivaa Prisons. Kwa sasa wanashika nafasi ya 15 na pointi tatu.




