Timu za Tanzania zaendelea kugawa dozi michuano FEASSSA 2024

TIMU za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Shule za Msingi na Sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA) zimeendelea kung’ara kwa kugawa dozi kwa timu pinzani katika michezo mbalimbali inayofanyika Mji wa Mbale nchini Uganda.

Michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Bukedea Mjini humo, Agosti 21, 2024, Timu ya Soka ya wasichana ya Tanzania imeibuka kidedea kwa kuicharaza Uganda mabao 5-0 huku Timu ya wavulana ikichapa Kenya mabao 4-0.

Katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya wasichana Tanzania imeibuka kidedea kwa kuifunga Kenya mabao 66- 62 huku mchezo wa wavu, timu ya wasichana Tanzania imeichapa Kenya seti 3- 1.

Pamoja na michezo hiyo, katika mchezo wa mpira wa mikono timu ya wasichana imeifunga Uganda mabao 20-15.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *