Washiriki 100 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wamethibitisha kushiriki kongamano la maendeleo ya mchezo wa kuogelea litakalofanyika Novemba 22 katika ukumbi wa PSSSF Tower, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ufundi wa TSA, Jeremiah Keema alisema kongamano hilo litajadili safari ya mchezo huo na muelekeo wake.
Wazungumzaji mbalimbali wakiongozwa na Rais wa TSA, David Mwasyoge na Mkurugenzi wa Ufundi Amina Mfaume watatoa mada.
Dirisha la usajili limefungwa na washiriki wametakiwa kufika mapema.




